MTAALAMU wa masuala ya ujenzi wa barabara, Bahati Mbambe amekosoa mfumo
wa ujenzi wa barabara nchini kwa kutowashirikisha wataalamu na
wakadiriaji majenzi (QS) kuwa unafanya barabara nyingi zinazojengwa
nchini kutokuwa katika vipimo sahihi.
Akitoa mhadhara mwishoni mwa wiki kwa wakadiriaji majenzi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam, Mbambe ambaye ni Mtanzania anayefanya kazi katika nchi mbalimbali za Kiafrika, alisema wakadiriaji majenzi ni wataalamu wanaotakiwa kuingizwa katika kila fani ya ujenzi inayofanyika nchini.
Wizi wa kupunja vipimo unaofanywa na makandarasi wa barabara uliwahi kulalamikiwa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, lakini katika mhadhara huo, mtaalamu huyo alisema kukomesha tatizo hilo, Serikali sasa iwashirikishe wakadiriaji majenzi katika ujenzi wa barabara zinazojengwa nchini.
Alisema ndio fani pekee ambao ni mabingwa wa kusoma namba wakati wahandisi wanahusika zaidi na masuala ya kiufundi; hivyo akataka mamlaka zinazohusika kurekebisha mfumo uliopo nchini ili wataalamu waliosomea masuala ya usanifu majengo wawe wanashirikishwa katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara.
“QS ndio fani pekee ambayo unaweza kufanya kazi kokote duniani katika sekta ya ujenzi mkubwa wa majengo, barabara, madaraja, kwenye kilimo na hata kwenye madini,” alisema Mbambe na kuwaambia wataalamu hao kuwa hawakukosea kusoma fani hiyo kwani wako katika njia sahihi. Mbambe ni Mtanzania aliyewahi kufanya kazi katika nchi za Mali,
Ghana, Cameroon, Chad, Guinea, Niger, Rwanda, Kenya, Benin na kwa sasa anafanya kazi katika mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Sumbawanga kwenda Laela mkoani Rukwa. Alisema alipokuwa anaangalia nyaraka zinazotoa mwongozo wa ujenzi wa mtandao wa barabara kuu nchini, alishangaa kuona kuwa wasanifu majengo wa Kitanzania hawashirikishwi sehemu yoyote katika kuandaa nyaraka hiyo ambayo ndio mwongozo wa ujenzi wa barabara kuu za hapa nchini. Alisema nyaraka hiyo kwa sasa inaandaliwa na Wakala wa Barabara (Tanroads) kwa kushirikiana na wataalamu wa mikoani peke yao wakati katika nchi zingine zikiwemo zilizoendelea wasanifu majengo ni lazima washirikishwe hasa katika suala la kuhakiki vipimo vya barabara.
source http://habarileo.co.tz/kitaifa/